Shirika la habari AhlulByt (a.s) ABNA: idadi kubwa ya wananchi wa mji wa New York na Washigton wamefanya maandamano ya kupinga hatua ya Rais mpya wa nchi hiyo ya kuzuia wahajiri wa kislamu kuingia nchini humo.
Waadamanaji hao walikuwa na mabango yalioandikwa ujumbe mbalimbali unaoashiria kuto ridhishwa na hatua ya Rais wa nchi hiyo ya kuwazuia wakimbizi wa Syria kuingia nchini humo, huku wakisisitiza kuchunga na kufuata haki za wahajiri nchini humo.
Aidha waandamanji hao katika maandamano ya Washngton ambao ni mmji mkuu wa Marekani, moja kati ya ujumbe uliokuwa umeandikwa katika mabango yao ni huu kwamba “sisi sote ni wahajiri” ambapo katika bando lingine limeandikwa “wakimbizi karibuni” huku wakisisitiza kuacha siasa hizo za kibaguzi.
Waandamanaji hao wameandamana huku wakitoa kauli mbiu yao kwamba, watu weusi, wakahawia, waeshia na wenye ngozi nyeupe wote wameungana kwaajili ya kutetea haki za wahajiri.
Moja kati ya mabango ya waandamanaji hao limeandikwa kwamba ”kuwa dhidi ya Muislamu ni sawa na kuwa dhidi ya Marekani”, pia katika maandamano hayo baadhi ya watu walipewa nafasi ya kuzungumza kwaajili ya kutetea haki za wahajiri. 










mwisho/290